Eneo la Keko Magereza #TPS SACCOS

Maswali na majibu Kuhusiana na Huduma Zetu

i) Je ni viambatanisho gani vinahitajika ili niweze kupata mkopo wa dharura?
Ili mwanachama aweze kupata mkopo wa dharura anatakiwa aandike barua ya maombi ya mkopo,ajaze fomu ya mkopo wa dharura kikamilifu,ajaze fomu ya mkataba kikamilifu,vile vile hati ya mshahara(salary slip) iambatanishwe.

ii)Je ni viambatanisho gani vinahitajika ili niweze kupata mkopo wa maendeleo?
Ili mwanachama aweze kupata mkopo wa maendeleo anatakiwa kuandika barua ya maombi ya mkopo,ajaze fomu ya maombi ya mkopo wa maendeleo kikamilifu,ajaze fomu ya mkataba wa mkopo wa maendeleo kikamilifu kisha aambatanishe hati ya mshahara(salary slip).

iii)Je ninaweza kukopa mkopo wa dharura ikiwa bado nina mkopo mwingine wa dharura unaoendelea?
Mwanachama anaweza kukopa mkopo mwingine wa dharura kama ana mkopo mwingine wa dharura unaoendelea ikiwa tu kama ameshalipa asilimia 75 ya mkopo wa awali.

iv)Je ninaruhusiwa kupunguza akiba mara ngapi kwa mwaka na ni kiasi gani naruhusiwa kupunguza?
Zoezi la kupunguza akiba limesitishwa kwa sasa na chama kimeanzisha utaratibu wa akaunti ya amana ambapo mwanachama anaweza kuweka amana yake na kuitoa muda wowote atakaotaka kufanya hivyo.

v)Je kiasi ninacho weka katika akaunti ya amana ninaweza kukitumia kama dhamna ya mkopo?
Kiasi unachoweka katika akaunti ya amana hakiwezi kutumika kama dhamana ya mkopo.

vi)Je TPSSACCOS inakopesha kama zinavyokopesha benki kwa kuangalia hati ya mshahara tu?
Kukopa Tpssaccos mkopaji anaruhusiwa kukopa mpaka mara tatu ya akiba yake.Hati ya mshahara inatumika kuangalia kiasi gani mkopaji anaweza kufanya marejesho kupitia mshahara wake.

vii)Je ninaweza kukopa mkopo wa maendeleo ikiwa nina mkopo wa dharura unaoendelea?
Mwanachama anaweza kukopa mkopo wa maendeleo hata kama ana mkopo wa dharura unaoendelea.