TPS SACCOS LTD imejengeka katika mwenendo wa ushirika wa akiba na mikopo kwa watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara, umejengeka katika maadili ya kusaidia, kuwajibika, demokrasia, usawa na haki, Wanachama wanaamini katika maadili ya ukweli, uwazi, uaminifu, uwajibikaji kijamii na kusaidia wengine.
Huu ni mkopo unaotolewa kwa mwanachama ambaye amepatwa na tatizo lolote linalohitaji ufumbuzi/utatuzi wa haraka.
Mkopo huu hautazidi shilingi milioni mbili na marejesho yake hayatazidi miezi kumi na miwili.Mkopo huu mwanachama atalipa kwa kukatwa moja kwa moja kutoka kwa muajiri wake au kwa kulipa fedha taslimu katika ofisi za chama au katika akaunti za benki za chama na kuwasilisha stakabadhi ya malipo hayo katika ofisi za chama.
+255 22 2865223 Wasiliana Nasi
Ni mkopo ambao anapewa mwanachama aliyepungukiwa akiba. Mkopo huu unamruhusu mwanachama kukopa zaidi ya akiba alizonazo ili mradi awe na sifa ya kurejesha mkopo huo .Sehemu ya mkopo itajazia katika akiba ya mwanachama ili aweze kukldhi vigezo. Vigezo na masharti mengine yanakuwa sawa na mkopo wa maendeleo.
+255 22 2865223 Wasiliana Nasi
Ni mkopo ambao mwanachama ataruhusiwa kukopa mkopo usiozidi mara tatu ya akiba zake pasipo kuathiri matakwa ya sheria ya ushirika Na.6 ya mwaka 2013 na kanuni zake.Mkopo huu unatolewa kwa riba ya asilimia kumi kwa mwaka kwa njia ya ulalo (Reducing balance method).
.
+255 22 2865223 Wasiliana Nasi
Amana ni fedha ambayo mwanachama anaweka katika chama chake kila anapokuwa na fedha ambayo haitaji kuitumia kwa wakati huo na fedha hiyo hurusiwa kuichukua muda wowote wa kazi.
+255 22 2865223 Wasiliana Nasi
Hisa ni sehemu ya umiliki wa mtaji wa chama ambayo inaweza kumilikiwa na mwanachama lakini haitakiwi kuzidi asilimia ishirini (20%) ya mtaji hisa ya chama
Akiba Ni kiasi cha fedha kinachowekwa na mwanachama ambacho kinatumika kama kigezo kwa mwanachama kupata mkopo kwa kuzingatia masharti yaliyoainishwa na fedha hiyo inaweza kuchukuliwa au kutumika kama dhamana ya kupata mkopo
Amana ni fedha ambayo mwanachama anaweka katika chama chake kila anapokuwa na fedha ambayo haitaji kuitumia kwa wakati huo na fedha hiyo hurusiwa kuichukua muda wowote wa kazi
Mwanachama ataruhusiwa kupewa mkopo usiozidi mara tatu (3) ya akiba zake pasipokuathiri matakwa ya sheria ya vyama vya ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 na Kanuni zake