Huduma za Tanzania Prisons Staff Saccos
i) Mkopo wa Dharura
Huu ni mkopo unaotolewa kwa mwanachama ambaye amepatwa na tatizo lolote linalohitaji ufumbuzi/utatuzi wa haraka. Mkopo huu hautazidi milioni moja na marejesho yake hayatazidi miezi kumi na miwili.Mkopo huu mwanachama atalipa kwa kukatwa moja kwa moja kutoka kwa muajiri wake au kwa kulipa fedha taslimu katika ofisi za chama au katika akaunti za benki za chama na kuwasilisha stakabadhi ya malipo hayo katika ofisi za chama.
ii)Mkopo wa maendeleo
Ni mkopo ambao mwanachama ataruhusiwa kukopa mkopo usiozldl mara tatu ya akiba zake pasipo kuathiri matakwa ya sheria ya ushirika Na.6 ya mwaka 2013 na kanuni zake.Mkopo huu unatolewa kwa riba ya asilimia kumi kwa mwaka kwa njia ya ulalo (Reducing balance method).
iii)Mkopo wa kupumulia
Ni mkopo ambao anapewa mwanachama aliyepungukiwa akiba .Mkopo huu unamruhusu mwanachama kukopa zaidi ya akiba alizonazo ili mradi awe na sifa ya kurejesha mkopo huo .Sehemu ya mkopo itajazia katika akiba ya mwanachama ili aweze kukldhi vigezo. Vigezo na masharti mengine yanakuwa sawa na mkopo wa maendeleo.